Matukio kama haya ya kiroho yanachochea kuenzi wapendwa wetu waliotangulia mbele ya Haki kwa njia ya kusimamisha Majlis, Dua, pamoja na kukuza upendo wetu na Ukaribu wetu kwa Kitabu Kitukufu cha Allah - Qur’an Tukufu - ambacho ni mwanga wa mioyo na njia ya wokovu kwetu.

2 Agosti 2025 - 05:12

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) - ABNA- Leo hii Jumamosi, tarehe 2 Agosti 2025, imefanyika ya Majlisi ya kumuombea rehema na maghfira Marehemu Sheikh Abdullah Khamis, mmoja wa wapenzi na watumishi wa Dini ya Kiislamu. 

Majlis ya Kuhitimisha Kisomo cha Qur’an Tukufu kwa ajili ya kumrehemu Sheikh Abdullah Khamis Yafanyika Katika Chuo cha Jamiatu Al-Mustafa(s)- Tanzania

Majlis hiyo ya kiroho ilitanguliwa na Kisomo cha Kuhitimisha Qur’an Tukufu kwa ukamilifu, na ilihudhuriwa na Waumini, Walimu, Wapenzi wa Qur'an Tukufu, Wanafunzi wa Chuo cha Jamiatu Al-Mustafa (s), Jijini Dar es Salaam, Tanzania.

Majlis ilifunguliwa kwa Kisomo cha Aya Tukufu za Qur’an kutoka kwa baadhi ya wasomaji mahiri wa Qur'an Tukufu na ambao ni Wanafunzi wa Chuo hiki, kisha washiriki wakaendelea kwa kusoma Qur’an yote kwa ushirikiano hadi kukamilika.

Katika hitimisho la hafla, Dua ya Khatmul - Qur’an ilisomwa, na washiriki wakamuombea Marehemu Sheikh Abdullah Khamis Dua Njema ya Maghfira, Msamaha, daraja ya juu Peponi, na Rehema za Mola wetu Mlezi.

Majlis ya Kuhitimisha Kisomo cha Qur’an Tukufu kwa ajili ya kumrehemu Sheikh Abdullah Khamis Yafanyika Katika Chuo cha Jamiatu Al-Mustafa(s)- Tanzania

Matukio kama haya ya kiroho yanachochea kuenzi wapendwa wetu waliotangulia mbele ya Haki kwa njia ya kusimamisha Majlis, Dua, pamoja na kukuza upendo wetu na Ukaribu wetu kwa Kitabu Kitukufu cha Allah - Qur’an Tukufu - ambacho ni mwanga wa mioyo na njia ya wokovu kwetu.

Your Comment

You are replying to: .
captcha